Header Ads

THIS ARE THE OTHER KENYAN VIP'S WHO HAVE PREDICTED THEIR DEATHS LIKE JACOB JUMA,PRAY FOR THEM

The death of Jacob Juma has without a doubt led to many questions and will in the days to come keep on churning theories upon theories on the reason why he was killed as well as those who killed him. What is not in doubt is the danger many outspoken individuals are facing. Mohammed Ali, one of the most celebrated and outspoken journalists seems to have been reminded of the threat to his person and has gone out to write a letter to the public on not just the threats he faces but also what he would love to happen in the event of his demise of incantation.
In his characteristic lengthy posts, Mohammed Ali who has been in recent times been more of an activist and a strong critic of the government of the day has been a thorn in the flesh for a number of the scrupulous government operatives and private businessmen he has exposed. Here is the chilling letter that has caused a fuss online; “NIKIFA KESHO WENGINE WAJASIRI WATAZALIWA. Huenda mada ya leo ikakutia hofu ama tumbo joto na kuwafurahisha wengine lakini usiwe na wasi wasi kwani kuzaliwa na kufa ni mapenzi yake Mwenyezi Mungu. Nikifa kesho msilie wala msinung’unike. Nikifutwa kazi kesho msiwe na chuki na mtu yeyote. Nikifungwa jela kesho msilie maana hii ndio safari ya mwanadamu ya kila siku. Msilie maana tulipofika sasa kama taifa tutalengwa wachache tunaopinga dhulma za kila siku. Tutalengwa wachache wanaopiga vita dhidi ya ufisadi. Tutalengwa kwa sababu tumekataa kuabudu miungu midogo midogo inayozidi kubaka taifa hili. Tutazidi kulengwa kwa sababu tumekataa kula meza moja na wabakaji wa demokrasia. Leo hii waandishi wa habari wanakamatwa kiholela na polisi kwa sababu ya kufichua uhuni wa baadhi ya viongozi wanaojifanya watumishi wa wakenya ilhali tabia zao ni kama panya buku. Tabia ya kung’ata na kupuliza. Wanahabari wanaachishwa kazi katika njia isiyoeleweka kwa sababu ya kusimama imara na kupinga maovu ya serikali. Sisi tayari tumetia kichwa chetu maji kukabiliana na lolote lile litakalojiri kwa ajili ya kusimama na wakenya. Leo kila mmoja wetu aliye katika taaluma hii ni mlengwa. Aliye katika afisi za serikali na anayepinga ukabila na wizi wa mali ya umma analengwa. Wengi wetu tunalengwa na kuzimwa ki-talanta kupitia wahuni wachache wanaojifanya wakubwa ila wao hawana tofauti na wale wanaobaka taifa hili, kwani ufadhili wa senti haramu za kuwapotosha wananchi kupitia taarifa bandia ndio kazi zao. Lakini leo nina habari njema kwa wakenya. Msiogope maana riziki yatoka kwake Mungu. Msiogope maana Mungu ni mkuu. Msiogope kudai haki zenu, mali yenu na uongozi mnaotaka. Msiogope kufutwa kazi kwa sababu ya kuunga mkono mabadiliko ya kweli. Hakika wengi wetu tutaumia katika safari hii ya kutetea nafasi yetu katika awamu ya tatu ya ukombozi wa Kenya. Awamu ya kuwaondoa wahuni wote mamlakani pamoja na wabakaji wa demokrasia. Mwaka wa 2017 utakuwa kama mwaka wa 2002 wakati ambapo vugu vugu litazaliwa kusafisha Kenya upya. Kesho ndio hiyo siku. Kesho yetu sote ni 2017. Kesho ni mimba ambayo imetungwa leo na yapaswa kujifungua. Twatarajia kujifungua mtoto mzuri aliyetungwa na atakaeleta mabadiliko na wala sio starehe. Wakenya wana maono sasa na hakuna mtu yeyote atakayejaribu kusimama mbele ya vuguvugu la mabadiliko. Wakenya wanataka waheshimiwe na kulindwa na wala si kuibiwa kila kukicha. Wakenya wanataka uongozi bora. Uongozi huo hautapatikana kwa kuwatesa baadhi ya watetezi wa haki za binadamu, wanahabari na wanasiasa wa upinzani. Hii itakuwa ni kosa kubwa kuwahi fanyika kwani wote hawa wanayafanya haya kwa minajili ya ukenya ndani yao na wala sio tamaa. Safari ya mabadiliko imeanza na hakuna aliye na nguvu ya kuzuia wanayoyataka wakenya. Safari hii itakuwa ya kiu, mateso na machungu lakini hakika dakika ya mwisho sote tutashinda. Sote tutaungana na kusimama kama taifa. Wakuachishwa kazi wataachishwa, wakufungwa jela watafungwa, wakuuawa watauawa, wakuteswa watateswa lakini Kenya itasimama imara baada ya safari hii. Safari ya kutafuta demokrasia huwa chungu na iliyojaa mitihani. GO TO PAGE 2 TO CONTINUE READING>>>>>>>>>> page 1 2
Powered by Blogger.